Nafasi za kazi
- Aug 18, 2020
- 1379 Views
- Job Vacancies
Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma ni Mamlaka ilioanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya kifungu nambari 4 cha Sheria ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma, namba 11 ya mwaka 2016, Jukumu kuu la kuanzishwa Mamlaka hii ni kusimamia utekelezaji bora wa Sheria ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma katika Taasisi /Idara zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuhakikisha uwepo wa thamani halisi ya fedha zinazotumika katika ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma pamoja na kuimarisha uchumi na ufanisi katika tathnia ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma.
Katika kuhakikisha inafanyakazi zake kwa ufanisi mkubwa, Mamlaka inahitaji nguvu kazi ya kutosha na yenye sifa ambayo itarahisisha kufikia malengo yaliyowekwa. Mamlaka inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo
Kwa upande wa Unguja
1 |
AFISA UJENGAJI UWEZO DARAJA LA II |
NAFASI 2 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
2 |
AFISA VIWANGO NA MIONGOZO DARAJA LA II |
NAFASI 2 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
3 |
AFISA UTAFITI DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
4 |
AFISA USHAURI DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
5 |
DEREVA DARAJA LA III |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
6 |
AFISA UTUMISHI DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
7 |
KATIBU MUHTASI DARAJA LA III |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
8 |
AFISA UFANISI NA UKIDHI WA MIKATABA DARAJA LA II
|
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
Kwa upande wa Pemba
1 |
MUHANDISI DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
2 |
AFISA TEHAMA DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
3 |
AFISA MIPANGO DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
4 |
DEREVA DARAJA LA III |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
5 |
AFISA UTUMISHI DARAJA LA II |
NAFASI 1 |
SIFA ZA MUOMBAJI
|
Jinsi ya kuomba
Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi za Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma Jengo la la Takwimu ghorofa ya pili Mazizini –Zanzibar kuanzia siku ya Jumatano ya tarehe 19/08/2020 saa mbili na nusu za asubuhi (2:30) hadi saa tisa na nusu za mchana (9:30) kwa anuani ifuatayo:
MKURUGENZI MTENDAJI
MAMLAKA YA UNUNUZI NA UONDOAJI WA MALI ZA UMMA
S.L.P 1290
MAZIZINI, ZANZIBAR.
Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma ilioko ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango Gombani chake chake Pemba.
Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi anayoomba vyenginevyo maombi yake hayatozingatiwa.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziambatanishwe na mambo yafuatayo:
- Cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
- Picha mbili za Paspot size zilizopigwa karibuni.
- Vyeti vya kumalizia masomo
- Kwa waombaji waliosoma Nje ya Nchi wanatakiwa waambatanisha na vyeti vyao vya TCU.
Atakaewasilisha ‘statement of result’ au ‘progressive report’, maombi yake hayatozingatiwa.
Mwisho wa kupokea maombi hayo ni siku ya Jumanne ya tarehe 25/08/2020 saa tisa na nusu (9:30) za mchana.